Marekani yasitisha mchango kwa kikosi cha amani Haiti
5 Februari 2025Marekani imesitisha mchango wake wa kifedha kwa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia shughuli za misheni yake ya kikosi cha kimataifa cha kusimamia amani nchini Haiti.
Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, hatua hiyo itasababisha kusitishwa kwa msaada wa dola milioni 13.3 zilizotegemewa kutolewa kwa kikosi hicho kinachoongozwa na Kenya.
Sooma pia: Marekani yasitisha kuchangia mfuko wa kusimamia kikosi cha kulinda amani Haiti
Baraza la usalama la Umoja huo wa Mataifa liliidhinisha Oktoba mwaka 2023, ujumbe huo wa kimataifa upelekwe kuisadia Haiti kupambana dhidi ya magenge ya wahalifu, wanaoyadhibiti maeneo mengi ya taifa hilo la Karribian.
Waziri wa mambo ya nje wa Haiti Jean-Victor Harvel Jean-Baptiste amesema nchi yake inakabiliwa na matatizo makubwa ambayo sio tu yanautatiza umma lakini pia yanatishia uhai wa nchi hiyo.