Marekani yasimamisha utoaji viza za wanafunzi wa vyuo vikuu
28 Mei 2025Hatua hiyo ndio ya karibuni katika ukandamizaji wa Ikulu ya White House dhidi ya wanafunzi wa kigeni, ambao umesababisha kufutwa viza na kufukuzwa nchini kwa baadhi ya waliohusika katika maandamano ya kupinga vita huko Gaza.
Soma pia:Trump aendelea kukisakama Chuo Kikuu cha Harvard
Taarifa iliyotiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio na kuoneshwa shirika la habari la AFP imeziamuru balozi kutomkubalia mwanafunzi yeyote wa ziada au viza za kipindi kifupi cha masomo hadi pale mwongozo mpya utakapotolewa.
Taarifa hiyo inasema serikali inapanga kuongeza uhakiki wa wasifu wa mitandao ya kijamii wa maombi ya kimataifa kwa vyuo vikuu vya Marekani. Japan na Hong Kong zimevihimiza vyuo vikuu vya ndani kuwakubalia wanafunzi wa kigeni kutoka vyuo vikuu vya Marekani kufuatia ukandamizaji huo.