SiasaSyria
Marekani yasifu makubaliano kati ya Syria na Wakurdi
12 Machi 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema wanayakaribisha makubaliano hayo yaliyotangazwa hivi karibuni kati ya mamlaka ya mpito ya Syria na kikosi cha wapiganaji wa Kikurdi nchini humo, SDF.
Mamlaka mpya za Syria chini ya Rais wa mpito Ahmed al-Sharaa zinanuia kusambaratisha makundi yenye silaha na kuweka udhibiti wa serikali nchini kote tangu Bashar al-Assad alipoondolewa madarakani mwezi Disemba.
Siku ya Jumatatu, ofisi ya rais wa Syria ilitangaza makubaliano na mkuu wa SDF ya kuunganisha taasisi za eneo linalojitawala la Wakurdi linalodhibiti sehemu kubwa ya kaskazini mashariki kwa muongo mmoja uliopita.