Marekani: Tutaendelea kuwashambulia waasi wa Kihouthi
17 Machi 2025Matangazo
Shirika la habari linalodhibitiwa na Wahouthi, SABA limeripoti kuwa mashambulizi mawili ya anga yamefanyika mapema leo kwenye eneo la mji wa bandari wa Hodeidah, ulioko umbali wa kilomita 230 kutoka mji mkuu wa Yemen, Sanaa.
Mashambulizi ya anga ya Marekani yaliyoanza Jumamosi dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na waasi hao kwenye miji ya Sanaa, Saada, Al-Bayda na Radaa, yamewaua watu 53 na kuwajeruhi wengine 101.
Soma pia:Marekani yalaani waasi wa Kihouthi kuwakamata wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa
Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth, amesema nchi hiyo itaendelea kuwashambulia waasi Houthi hadi watakapoacha kuzishambulia meli za kimataifa.