Marekani kubatilisha visa zote za raia wa Sudan Kusini
6 Aprili 2025Matangazo
Amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa kuwa taifa hilo la Afrika llimeshindwa kuwapokea raia wake waliofukuzwa Marekani. Rubio amefafanua zaidi kuwa, kila nchi inapaswa kuwakubali wananchi wake kwa wakati mara tu wanapofukuzwa na mataifa mengine ikiwemo Marekani lakini serikali ya mpito ya Sudan Kusini imeshindwa kuiheshimu kanuni hiyo.
Soma zaidi: Raia wa mataifa 43 kupigwa marufuku kuingia Marekani
Kutokana na hilo wizara yake imezuia pia kutolewa kwa visa mpya kwa wananchi wa taifa hilo ili kuwazuia wasifike Marekani. Hata hivyo Rubio amesema nchi yake iko tayari kutathmini upya uamuzi huo pale tu serikali ya Rais Salva Kiir itakapotoa ushirikiano.