Marekani yamuuwa mkuu mmoja wa kundi la kigaidi Syria
22 Februari 2025Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, jeshi hilo limesema kuwa vikosi vya Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) vilifanya mashambulizi ya anga kaskazini-magharibi mwa Syria, na kumuua Wasim Tahsin Bayraqdar, afisa mkuu wa kundi hilo la kigaidi la Hurras al-Din.
Takribani watu 15 wameua mlipuko wa bomu Syria
Eneo la kaskazini-magharibi mwa Syria lilikuwa ngome ya kundi la Hayat Tahrir al-Sham la rais wa mpito Ahmed al-Sharaa kabla ya kuongoza mashambulizi ya waasi yaliyomuondoa madarakani rais Bashar al-Assad mwezi Disemba mwaka jana.
Hilo ni shambulio la hivi karibuni zaidi la Marekani mwaka huu dhidi ya kundi hilo nchini Syria. Pamoja na washirika wake wa Magharibi na Kiarabu, Marekani imesisitiza kuwa Syria haipaswi kuwa eneo la makundi ya kigaidi baada ya kuangushwa utawala wa Assad.