Marekani yalaani Wahouthi kuwakamata wafanyakazi wa UN
26 Januari 2025Taarifa ya wizara hiyo imesema hatua yawaasi hao ya hivi karibuni inaonesha nia mbaya ya kundi hilo linalodai kutaka kupunguza mivutano na kulinda maslahi ya watu wa Yemen.
Mbali na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambao miongoni mwao ni waliokamatwa Alhamisi, Waasi wa Kihouthi wamewakamata wafanyakazi kadhaa wa mashirika ya kutetea haki za binadamu tangu katikati mwa mwaka 2024.
Soma zaidi: Wafanyakazi tisa wa UN washikiliwa na Waasi wakihouthi Yemen
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amatoa wito wa kuachiliwa kwa wanaoshikiliwa na waasi hao nchini Yemen. Wahouthi wanaosema wanaonesha mshikamano na Wapalestina wamekuwa wakizishambulia meli katika Bahari ya Shamu na kuilenga Israel tangu vita vilipoanza Gaza. Matokeo yake waasi hao wamekuwa wakipata mashambulizi ya kulipa kisasi kutoka kwa Marekani, Israeli na Uingereza.