Marekani yakiri kuweko matatizo ya usalama nchini Iraq
9 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Wanajeshi wa Kimarekani wamekabiliwa na njama za kiasi nchini Iraq, kwa mujibu wa Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Richard Armitage. Kule kuendelea kushambuliwa wanajeshi wake kunailetea Marekani matatizo makubwa ya usalama nchini Iraq, alisema Bwana Armitage wakati akiuzuru mji mkuu Baghdad. Wairaq wenyewe wanapaswa kuchukua dhamana zaidi ya kuhakikisha usalama wa ndani, alisisitiza. - Hapo jana iliendelea ile orodha ya mashambulio ya kigaidi nchini Iraq. Mjini Falluja waliuawa wanajeshi wawili wa Kimarekani katika shambulio la bomu. Na mjini Baghdad bomu liliripuka karibu ya makao makuu ya wanajeshi wa Kimarekani bila ya kutiwa hasara.