Marekani yajiondowa UNESCO
22 Julai 2025Matangazo
Marekani imetangaza leo Jumanne, kwamba kwa mara nyingine itajiondowa katika shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO.
Washington, ambayo iliwahi kujitowa na kisha kujiunga tena naUNESCO miaka miwili iliyopita, inaitazama taasisi hiyo kama chombo kinachoionea na kuichukia Israel.
Uamuzi wa Marekani wa kujiondowa kuwa mwanachama wa UNESCO utaanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka 2026. Hiyo itakuwa ni mara ya tatu kwa Marekani kujitenga na shirika hilo lenye makao yake mjini Paris na mara ya pili chini ya utawala wa Trump.