Asili na mazingiraAfrika Kusini
Marekani yajiondoa kufadhili miradi ya mazingira
6 Machi 2025Matangazo
Afrika Kusini ndio nchi ya kwanza kufaidika na mpango huo. Mpango huo unaofahamika kama JETP, unahusisha kundi dogo la mataifa tajiri na mataifa yanayoinukia kiuchumi kuyasaidia kuondokana na matumizi ya makaa ya mawe.
Afrika Kusini ambayo ina utajiri wa makaa ya mawe lakini yenye kiu ya nishati, ilikuwa ndio nchi ya kwanza katika mataifa yanayoendelea kujiunga na makubaliano hayo ya JETP mnamo mwaka 2021.
Marekani iliiahidi Afrika Kusini dola bilioni 12.8 chini ya mpango huo.