Marekani yataka Rwanda itoe wanajeshi DRC-Vyanzo
10 Juni 2025Marekani inaitaka Rwanda iwaondoe wanajeshi wake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kabla ya kusainiwa makubaliano ya amani.
Hayo yameelezwa na vyanzo ambavyo vimefafanuwa kwamba Marekani inaunga mkono makubaliano ambayo yataihitaji Rwanda kuchukua hatua hiyo ya kuondoka Mashariki mwa Kongo.
Sharti hilo laMarekanihuenda likaikasirisha Kigali ambayo inayaita makundi yenye silaha nchini Kongo kuwa kitisho cha kudumu kwa usalama wake. Serikali ya Rais Donald Trump inaendesha mazungumzo ya kumaliza vita mashariki mwa Kongo ili kuwekeza mabilioni ya dola kwenye eneo hilo lenye utajiri wa madini.
Rasimu ya mkataba wa amani iliyoonekana na shirika la habari la Reuters imebainisha kwamba sharti mojawapo lililoorodheshwa kabla ya kusainiwa, ni kwamba Rwanda inatakiwa kuondowa wanajeshi wake, silaha na vifaa kutoka Kongo.