Marekani yaipa Iran muda kumaliza miradi ya kinyuklea
14 Februari 2004Matangazo
WASHINGTON: Marekani imeipa Iran muda maalumu wa kumaliza miradi yake ya kinyuklea. Serikali mjini Teheran ina muda mpaka uanze mkutano ujao wa Shirika la Kimataifa la Kinyuklea (IAEO) hapo Machi 8 mwaka huu kutekeleza ahadi zake za kumaliza miradi yake ya kinyuklea, alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje mjini Washington. Ikiwa Iran haitoonyesha imani ya kushirikiana, basi serikali ya Marekani itashikilia kuwa swali hilo likabidhiwe Baraza la Usalama la UM na huko Iran inaweza kutarajia itachukuliwa hatua kali.