Marekani yafuta Viza kwa raia wa Sudan Kusini
7 Aprili 2025Matangazo
Utawala wa Marekani wa rais Donald Trump umetangaza kubatilisha visa za kusafiri nchini humo kwa raia wote wa kutoka Sudan Kusini, ikisema serikali ya Juba imekataa kuwapokea raia wake wanaorudishwa kutoka Marekani, kwa muda mwafaka.
Uamuzi huo unamaanisha raia wa Sudan Kusini walioko Marekani huenda wakarudishwa nyumbani ambako kwa mara nyingine kunashuhudiwa vita.Marekani yasema itabatilisha visa zote za raia wa Sudan Kusini
Sudan Kusini ambayo kuundwa kwake kama taifa huru mwaka 2011 kuliungwa mkono na Marekani hivi sasa iko ukingoni kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hadi sasa serikali ya mjini Juba haijatowa tamko kuhusu hatua ya Marekani.