Migogoro
Marekani yafanya mashambulizi katika maeneo ya Yemen
19 Machi 2025Matangazo
Vyombo vya habari nchini Yemen vimeripoti kwamba jeshi la Marekani limefanya mashambulizi 10 yaliyolenga maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo, Sanaa, na mji wa bandari wa Hodeidah hivi leo.
Marekani ilianzisha wimbi jipya la mashambulizi katika maeneo ya Yemen yanayodhibitiwa na Wahouthiwanaoungwa mkono na Iran, ambao walisema wiki iliyopita kwamba wangelianzisha tena mashambulizi dhidi ya meli za Marekani katika Bahari ya Shamu ili kuwaunga mkono Wapalestina wanaoshambuliwa kwenye Ukanda wa Gaza.
Katika hatua nyingine, msemaji wa kundi la hilo la wanamgambo wa Kihouthi amesema leo kwamba wamefanya mashambulizi mapya manne leo yanayolenga meli za kivita za Marekani katika Bahari ya Shamu katika kipindi cha masaa 72 yaliyopita.