Marekani yaepuka kufungwa kwa shughuli za serikali
15 Machi 2025Matangazo
Marekani imeepuka kufungwa kwa shughuli za serikali kukiwa kumebaki saa chache Ijumaa huku wabunge waliokuwa tayari wakiyumba kutokana na hatua za rais Donald Trump kubana matumizi makubwa ya fedha wakipiga kura kuruhusu matumizi hadi Septemba.
Wakikabiliwa na muda wa mwisho saa sita usiku saa za Marekani kuipa fedha serikali au ianze kufunga shughuli zake, wabunge wa chama cha Democratic waliachana na mipango ya kuuzuia muswaada unaoungwa mkono na Trump uliopitishwa mapema wiki hii na baraza la wawakilishi, na kuusafishia njia uidhinishwe na baraza la seneti linaloongozwa na chama cha Republican.
Mwenyekiti wa kamati ya biashara ya baraza la seneti Ted Cruz amesema serikali sasa imefadhiliwa na kutoa wito kwa Wamarekani warejee kazini.