Uchumi
Marekani yaanza kuiondolea Syria vikwazo vya kiuchumi
24 Mei 2025Matangazo
Kulingana na wizara ya fedha ya Marekani ni kwamba kuondolewa vikwazo hivyo, kutaruhusu shughuli mpya za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha na shughuli zinazohusiana na mafuta ya petroli na bidhaa za petroli zinazotoka nchini Syria.
Marekani itarejesha pia ushirikiano na serikali mpya, na rais wa mpito Ahmed al-Sharaa, benki kuu ya Syria na taasisi zingine za kifedha. Aidha, Washington itabakisha vikwazo dhidi miamala inayoinufaisha Urusi, Iran au Korea Kaskazini.
Wiki iliyopita, Trump alitangaza kuondolewa kwa vikwazo vyote vya Marekani, vilivyowekwa chini ya utawala wa Bashar al-Assad, dhidi ya Syria.