MigogoroMashariki ya Kati
Marekani na Wahouthi waafiki kusitisha makabiliano
7 Mei 2025Matangazo
Hayo ni kwa masharti kwamba waasi hao wataacha kuzilenga meli za biashara kwenye ujia muhimu kimataifa unaokatisha Bahari Nyekundu.
Tangazo la kufikiwa makubaliano hayo limetolewa na wapatanishi wa Oman walioongoza juhudi za siku kadhaa za kidiplomasia.
Saa chache kabla ya tangazo hilo, Rais Donald Trump wa Marekani alisema nchi yake itasitisha kuwashambulia waasi wa Houthi baada ya kundi hilo kuridhia kutozighasi tena meli za mizigo.
Kwa karibu wiki saba zilizopita Washington imekuwa inafanya mashambulizi makali dhidi ya Wahouthi ndani ya Yemen ambayo yamesababisha vifo vya watu 300.
Hata hivyo viongozi wa Wahouthi wamesema pamoja na makubaliano hayo na Marekani, kundi hilo halitositisha mashambulizi yake yanayoilenga moja kwa moja Israel.