Marekani na Urusi zajadili usitishaji vita vya Ukraine
24 Machi 2025Maafisa wa Marekani na Urusi wamekutana nchini leo nchini Saudi Arabia kujadili usitishaji mapigano baada ya mazungumzo ya kwanza kati ya Marekani na Ukraine kukamilika hapo jana.
Timu ya wajumbe wa upatanishi wa Marekani na Urusizimekutana katika hoteli moja ya kifahari mjini Riyadhi. Miongoni mwa yaliyojadiliwa katika mazungumzo hayo ni pamoja kuufufua tena mpango wa usitshaji vita katika Bahari Nyeusi.
Akizungumzia mkutano huo, Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dimitry Peskov amesema.
"Kwa sasa tunazungumza juu ya nia na utayari wa nchi hizi katika kusonga mbele katika kutafuta suluhu ya amani. Hapa kuna maelewano ya pamoja kuhusu masuala ya kitalaamu, na kama unavojua kwamba masuala haya ya kitalaamu, yalikuwepo katika mazungumzo yaliyofanyika leo huko Riyadh kati yetu na ujumbe wa Marekani. Bila shaka, masuala mengi yanayohusiana na makubaliano bado yanahitaji kushughulikiwa."Wajumbe wa Marekani na Urusi wakutana Riyadh kutafuta suluhu ya vita vya Ukraine
Mapema Jumatatu, Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov alisema duru ya kwanza ya mazungumzo ambayo ilikamilika Jumapili jioni ilikuwa yenye tija na kutoa mwelekeo chanya.