Marekani na Urusi zabadilishana mawazo mapya kuhusu Ukraine
10 Julai 2025Taarifa iliyotolewa muda mfupi baada ya mkutano wa leo Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Urusi walibadilishana mawazo ya msingi na maoni ya wazi kuhusu masuala ya Ukraine, Iran, Syria, na migogoro mingine ya kimataifa.
Nchi zote mbili zimesisitiza ahadi yao ya pamoja katika kutafuta masuluhisho ya amani kwa mizozo, kurejesha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Urusi na Marekani, ushirikiano wa kibinadamu, na mawasiliano bila vizuizi kati ya jamii za nchi hizo mbili, jambo ambalo litawezeshwa kwa kuanzisha tena safari za ndege za moja kwa moja kati ya Marekani na Urusi.
Rubio na Lavrov, wamefanya mazungumzo kandoni mwa mkutano wa kila mwaka wa nchi 10 wanachama wa Jukwaa la Kikanda la Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN. Nchi washirika wa Jukwaa hilo ni Urusi, na China.