Migogoro
Marekani na Ufilipino zaanza luteka za kijeshi za wiki tatu
21 Aprili 2025Matangazo
Luteka hizo za kila mwaka maarufu kama Balikatan yaani "bega kwa bega" zinajumuisha wanajeshi 5,000 wa vikosi vya Ufilipino na elfu tisa vya Marekani. Luteka hizo zinaudhuriwa pia na wanajeshi kutoka Japan, Australia, Ufaransa, Uingereza, Jamhuri ya Czech, Lithuania, Poland na Uholanzi.
Silaha za kisasa za Marekani ikiwa ni pamoja na mfumo wa makombora wa kukabiliana na meli za kivita ya NMESIS pia zimepelekwa katika luteka hizo zitakazofanyika nchi kavu na baharini.