Marekani na Iraq zinatafuta njia za kuwazuwia mabalozi wa kigeni wasiondoke Baghdad
6 Julai 2005Iraq na Marekani zinatafuta njia za kuzuwia kuondoka wanadiplomasia wa kigeni kutoka Iraq. Mabalozi wa Pakistan na Bahrein walfyetuliwa risasi jana wakiwa katika magari yao, ikiwa ni siku tatu baada ya balozi wa Misri huko Baghdad, Ihab al-Shariff kutekwa nyara katika barabara ya mji mkuu wa Iraq. Kikundi cha mtandao wa al-Qaida huko Iraq kimesema kinamshikilia Bwana al-Shariff. Marekani imezihimiza nchi nyingine zisionshe mabalozi wao.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uengereza, Jack Straw, amesema majeshi ya Muungano huko Iraq yataondoka kutoka nchi hiyo punde paleyatakapombwa kufanya hivyo na serekali ya nchi hiyo. Akizungumza mbele ya Bunge la Ulaya mjini Strassbourg, Bwana Straw alisema, kimsingi, hana matatizo ikiwa majeshi ya Umoja wa Mataifa yatakuweko Iraq. Hata hivyo alisema ni shida harakati kama hizo za Umoja wa Mataifa kuungwa mkono. Alikiri juu ya hali mbaya ya usalama katika Iraq na akasema suluhisho lililo bora ni kwa majeshi ya kigeni kupunguzwa na badala yake yawekwe majeshi ya Ki-Iraqi.