Iran na Marekani zatofautiana kuhusu athari ya mashambulizi
25 Juni 2025Matangazo
Mshauri wa mambo ya nje wa ikulu ya Urusi Yuri Ushakov amesema nchi yake imekaribisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya pande hizo mbili hasimu, na inatumai yatadumu.
Amesema lakini kuna taarifa kinzani juu ya kiwango cha uharibifu.
Bunge la Iran lapitisha mswada wa kusimamisha ushirikiano na shirika la kuratibu masuala ya nyuklia
Amesema Aliyeshambulia ambaye ni Marekani anadai kuviharibu kabisa vinu hivyo na aliyeshambuliwa anaamini kwamba kila kitu kiliratibiwa mapema na kwamba uharibifu haukuwa mkubwa kama Marekani inavyodai.
Urusi imesema ni mapema mno kwa yeyote kuwa na picha halisi ya uharibifu uliosababishwa.