SiasaIran
Marekani na Iran kufanya mazungumzo ya Nyuklia
9 Aprili 2025Matangazo
Washington na Israel zimeonya kuchukua hatua za kijeshi endapo mazungumzo kati ya mataifa hayo yatadorora. Mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika Oman yanaonekana kuwa juhudi mpya ya kurejesha maelewano na kuepusha mzozo wa kijeshi.
Soma pia:Iran: Hatutaki mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani
Tangu kujiondoa kwa rais wa Marekani Donald Trump katika makubaliano ya kihistoria ya mwaka 2015 yaliyopunguza vikwazo kwa masharti ya kudhibiti mpango wa nyukliawa Iran mvutano kati ya Marekani na mataifa ya magharibi umeongezeka.
Hata hivyo mazungumzo mapya kati ya Washington na Tehran yanasubiriwa kwa hamu, wakati hofu ya kuibuka matumizi ya silaha za nyuklia ikiendelea kutanda.