Marekani na Colombia zazozana kuhusu kufukuzwa wahamiaji
27 Januari 2025Hatua hiyo inadhihirisha kile ambacho nchi mbalimbali huenda zikakabiliwa nacho kama zitaingilia msako unaofanywa na utawala wa Trump dhidi ya uhamiaji haramu. MaraisDonald Trump na Gustavo Petro wametetea misimamo yao kuhusu uhamiaji, huku Petro wa Colombia akimtuhumu Trump kwa kutoonesha utu kwa wahamiaji wakati wa kuwafukuza nchini.
Petro alitangaza ongezeko la asilimia 25 ya ushuru kwa bidhaa za Marekani. Awali, Rais wa Marekani aliamuru vikwazo vya viza, ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zote za Colombia zinazoingizwa nchini, ambao utaongezwa hadi asilimia 50 katika wiki moja, na hatua nyingine za kulipiza kisasi. Ni baada ya Rais Petro kukataa kuruhusu ndege mbili za kijeshi za Marekani zilizokuwa na wahamiaji wa Colombia kutua nchini humo. Trump alisema hatua hizo zilihitajika ka sababu uamuzi wa Petro ulihatarisha usalama wa kitaifa nchini Marekani.