Marekani na China zakubali kupunguziana ushuru
12 Mei 2025Hisa katika masoko ya biashara zimepanda leo Jumatatu baada ya Marekani na China kufanya mazungumzo ya kibiashara yaliyokuwa na tija.
Mataifa hayo mawili yalikubaliana na kutangaza kupunguza ushuru wa ziada kwa siku 90, hatua iliyochochea matumaini kwamba pande hizo mbili hatimae zitamaliza mvutano wao uliosababisha mtikisiko kwenye masoko ya dunia.Soma pia: Wawakilishi wa China na Marekani wakutana kujadili namna ya kutuliza mvutano wa kibiashara
Baada ya mazungumzo ya siku mbili mjini Geneva, nchini Uswisi, Marekani na China zimetowa taarifa ya pamoja ambapo inaonesha kwamba Marekani imekubali kuipunguzia China Ushuru hadi asilimia 30 huku China nayo ikiipunguzia Marekani ushuru hadi asilimia 10 kuanzia leo Jumatatu.
Muda wa siku tisini utatumiwa na maafisa wa pande zote kushughulikia tofauti zilizopo.