Marekani kuwapa makazi Waafrika Kusini wa asili ya kizungu
9 Mei 2025Matangazo
Utawala wa rais Donald Tump unapanga kuwapa makazi nchini Marekani kundi la kwanza la wazungu raia wa Afrika Kusini wiki ijayo.
Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani baada ya rais Tump kuituhumu Afrika Kusini kwa ubaguzi wa rangi dhidi yao.
Trump yuko katika mgogoro wa kidiplomasia na Afrika Kusini kuhusu sheria ya unyakuzi wa ardhi ambayo anasema itapelekea mashamba ya wazungu raia wa Afrika kuchukuliwa na serikali.
Radio ya Taifa NPR na gazeti la New York Times viliripoti hapo jana kwamba kundi la kwanza la Waafrika Kusini weupe limepangwa kuwasili Jumatatu ijayo, ingawa gazeti hilo liliwanukuu maafisa wakisema tarehe hiyo inaweza kubadilika kulingana na mipangilio.