Marekani kujenga kituo cha kwanza cha wahamiaji Texas
8 Agosti 2025Matangazo
Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon imesema hapo jana kwamba mpango wa awali ni kuwapa hifadhi wahamiaji 1,000 katika kambi ya jeshi la Fort Bliss karibu na mpaka na Mexico kuanzia mwezi huu.
Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi kituo hicho kilichopewa jina la Camp East Montana, baadaye kitatanuliwa kutoa huduma za malazi na vitanda kwa wahamiaji 5,000 katika wiki na miezi inayokuja.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vikiinukuu idara ya uhamiaji na utekelezaji wa forodha wizara ya ulinzi inafadhili kituo hicho cha kuwazuilia wahamiaji kitakachojumuisha nyumba za muda mfupi mfano wa mahema.