Marekani kubadili Plani ya Iraq:
17 Januari 2004WASHINGTON:
Marekani itayari kubadili plani yake ya
kuikabidhi madaraka serikali mpya ya Iraq,
alisema Mtawala wa Kimarekani wa Mambo ya
Kiraiya mjini Baghdad. Majeshi Shirika
yanayoongozwa na Marekani daima yamekuwa
tayari kuyabadili mawafikiano hayo
yaliyofikiwa katikati ya Novemba na
kuyatangaza wakati muwafaka, alisema mtawala
huyo Paul Bremer baada ya kukutana na Rais
George W. Bush mjini Washington. Kuna
uwezekano wa kufanywa mabadiliko katika
uteuzi wa Bunge la Mpito litakaloichagua
serikali halisi ya Iraq, alisema.- Kiongozi
wa Kishiya wa Kiiraq Ayatollah Ali el Sistani
ametoa mwito wa kufanyika uchaguzi wa mapema
na wa moja kwa moja kuwawezesha raiya
kuichaguwa serikali huru. Mapatano
yaliyofikiwa hapo katikati ya Novemba
yanaahidi tu uteuzi wa bunge la mpito
litakaloichagua serikali.