Marekani inapanga kuwaunga mkono kifedha wapenda kidemokrasia nchini Iran
12 Aprili 2005Teheran
Serikali ya Iran imekosoa vikali uamuzi wa Marekani wa kuyapatia fedha makundi ya upinzani ili kuimarisha demokrasia nchini humo.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, Iran inapanga kuishitaki Marekani mbele ya mahakama ya kimataifa mjini The Hague.Serikali ya Iran inasema Marekani kwa kufanya hivyo inakwenda kinyume na sheria za kimataifa.Hapo awali serikali ya Marekani ilisema kinaga ubaga inapanga kutoa fedha kusaidia juhudi za kuleta kidemokrasia nchini Iran.Itakua mara ya kwanza kwa serikali ya Marekani kufanya hivyo tangu miaka 25 iliyopita.Dola milioni 3 zimetengwa kwa sasa kwaajili hiyo.Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje Richard Boucher amezisuta hoja za serikali ya Iran.Amedai Marekani inaunga mkono demokrasia na haki za binaadam kote ulimwenguni.Serikali ya Iran inahoji kwa kutoa fedha hizo Marekani inaingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo .