Marais wa Uturuki na Syria wafanya mazungumzo mjini Istanbul
24 Mei 2025Matangazo
Wiki hii maafisa wa Uturuki na Syria walikuwa na mazungumzo mjini Damascus kuhusu zoezi la kundi la wanamgambo wa Kikurdi wa YPG huko Syria kuweka silaha chini na kujiunga na vikosi vya usalama vya Syria.
Ziara hiyo inakuja siku moja baada ya utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi Syria.
Wiki iliopita, Trump aliahidi kuondoa vikwazo hivyo ili kuisaidia Syria kujijenga upya baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoharibu taifa hilo.